Search This Blog

Nyumbani-Kigoma All stars

MAHAKAMA YA MAPENZI

Tuesday, October 30, 2012

SISI SI FREEMASON-P-SQUARE

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kufuatia tuhuma mbalimbali ikiwemo kumuua mama yao ili kujipatia umaarufu pamoja na kuabudu katika dini ya shetani maarufu kama freemason ,Mapacha wa kinijeria wanaotamba kwenye muziki na wenye mafanikio makubwa kiuchumi Peter na Paul Okoye,Wameibuka na kuziita tuhuma hizo ni upuuzi mtupu,

KUMUUA MAMA YAO
                           Peter na Paul wakiwa wamebeba jeneza la mama yao alizikwa  2/8/2012
Kulikuwa na stori nyingi kuwa walimuua mama yao ili kujipatia umaarufu na kujiongezea utajiri.Vijana hao wamekana tuhuma hizo na kusema huo ni upuuzi kwani mama yao alikuwa muhimu kuliko umaarufu na fedha."ni jambo  baya kusikia watu wakituhusisha na kifo cha mama,huwezi kumlaumu mtu yeyote lakini waache waongee kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya hivyo....Maisha ya mama hayawezi kufananishwa na  fedha wala umaarufu"

KUWA FREEMASON
"Pia ni upuuzi kusema sisi ni wanachama wa nguvu za giza(freemason)huo ni uongo na hatumilikiwi na kikundi chochote....Tunamwamini  Mungu"Hayo ni maneno aliyozungumza  Peter  pacha mkubwa wa Paul.
P-squre wamekuwa gumzo kuwa wanachama  wa  freemason kufuatia kuwa vizuri kiuchumi  na pia kufanya kolabo na Rick Rose ambaye inasemekana usipokuwa mwanachama wa freemason huwez kufanya nae kolabo.