Search This Blog

Nyumbani-Kigoma All stars

MAHAKAMA YA MAPENZI

Friday, February 12, 2016

NEY AWAKEJELI BASATALICHA ya kufungiwa kwa wimbo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego uitwao Shika adabu yako, msanii huyo ameonekana kutojutia uamuzi huo uliotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

SIKU 100 ZA UTENDAJI WA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI


LEO ni siku ya 100 tangu Rais John Magufuli alipoingia Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam, na tangu alipotoa hotuba yake siku ya kuapishwa na ile ya uzinduzi wa Bunge la 11, ameishi katika maneno yake kwa kutenda kile anachokisema.
Miongoni mwa mambo aliyoahidi ni kupambana na rushwa pamoja janga la dawa za kulevya, akisema dawa za kulevya zimeathiri vijana wengi, hivyo akaahidi kushughulikia mtandao huo na wakubwa wanaohusika. Kwa upande wa rushwa, Rais Magufuli aliahidi kupambana na ufisadi na rushwa na katika kutekeleza hilo, alisema ataunda mahakama maalumu ya kushughulikia wezi wakubwa yaani mafisadi. Pia aliahidi kuwashughulikia wafanyakazi wazembe ili Serikali yake isiendelee kulea watu wanaolipwa mishahara tu wakati hawafanyi kazi yoyote.
Katika kubana matumizi ya serikali, aliahidi kudhibiti warsha ambazo hazina umuhimu katika Serikali wala kuongeza ufanisi kwa wafanyakazi. Aliahidi pia kudhibiti safari za nje, ambazo zimekuwa zikigharimu Serikali fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Rais Magufuli pia alisema Serikali yake itaongeza wigo katika ukusanyaji wa mapato, ukizingatia kuwa kodi ni kitu muhimu na ni lazima zikusanywe.
Aliahidi kufufua viwanda viliyobinafsishwa, ambavyo baadhi alidai vimegeuzwa mazizi ya mbuzi wakati waliopewa kwa madhumuni ya kuviendeleza. Aliahidi pia kushughulika na kero zinazolalamikiwa kutendwa na polisi, hospitali, mizani, Mahakama, maliasili na vilio vya wachimbaji. “Inabidi haya yote niyataje ili nijue tunaanzia wapi na tunakwenda wapi, nisipoyataja nitakuwa mnafiki,” alisema Rais Magufuli wakati akizindua Bunge la 11 mjini Dodoma.