Search This Blog

Nyumbani-Kigoma All stars

MAHAKAMA YA MAPENZI

Wednesday, June 27, 2012

DOKTA ULIMBOKA ATEKWA APIGWA YUPO ICU

 Hii picha ikimuonesha Dr Ulimboka baada ya kuokotwa....
Dr Ulimboka akiwa katiak moja kati ya mikutano ya madaktari
Kiongozi wa madaktari Dr Steven Ulimboka  ameokotwa leo asubuhi eneo la msitu wa Mwabe pande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam  huku akiwa ameumia vibaya sana.Mpaka tunarusha taarifa hii inasemekana Dr Ulimboka yupo icu katika hospitali ya taifa Muhimbili huku akiwa hapumui vizuri...Dr ulimboka anayejulikana kwa misimamo yake na kupigania haki za madaktari alitekwa majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo na inasemekana amevunjika pia mkono,taya na kuumia vibaya sehemu nyingine za mwili wake...Wakati haya yakijiri serikali kesho itatoa msimamo juu ya mgomo wa madaktari unaoendelea kwa baadhi ya hospitali....Get well soon mpambanaji  Ulimboka

1 comment:

Anonymous said...

Bwana hiyo yote ni ftna ya serikali ya kikwete.. wanapomuita dhaifu asidhani hawezi kuzaa la hasha ila tu hawezi kuongoza wajukuu wa baba yake. Yaani wameshindwa juhudi zote za kidiplomasia na kuanza kutumia nguvu!!! Ulimboka pona mapema baba!!! Mungu anajua huna kosa lolote juu ya waliokupiga hivyo hataruhusu mauti ikufike ila OLE WAO WALIOMPIGA MAANA MATESO WATAKAYOPATA WAO NA FAMILIA ZAO HAYANA MFANO. Mtu anatetea madaktari walipwe vizuri ili wafanye kazi kwa moyo, kisha mnampiga!!Ni wapumbavu wachache waliokosa elimu ndo walofanya hivyo kwa tamaa za pesa ndogondogo. Mnashindwa kwenda kuwapiga majizi ya pesa za umeme maana waliwalaza giza miezi, wewe mama yako, Mkeo na watoto wako.. Eti kwa ujinga unapewa milionioni kadhaa.. kwenda kumuua mtu anayetetea afya ya mwanao. Kafie mbali wewe uliyeinua mkono wako kumpiga dokta Ulimboka.