Sakata la msanii maarufu Afrika mashariki la kuitapeli kampuni ya global publishers katika tamasha la matumaini lililofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar -es salaam,limechukua sura mpya baada ya
DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou ‘DJ JD’,jana nae alieweka wazi
utapeli aliowahi kufanyiwa miaka saba iliyopita na mwanamuziki raia wa
Uganda, mwenye hulka ya utapeli, Joseph Mayanja Chamelone.
DJ JD
JD,
amewaeleza waandishi wa habari leo, waliokusanyika kwenye Hoteli ya The
Atriums kwamba Chameleone siyo mtu mzuri anapokubaliana na mapromota,
kwani hata yeye aliwahi kumtapeli dola za kimarekani 3,000, mwaka 2005.
Erick Shigongo mkurugenzi wa global publishers akiwa na DJ JD na meneja wa kampuni yake Abdalah mrisho.
Alisema mbele ya waandishi wa habari: “Niliwasiliana na Chameleone
moja kwa moja, akanikubalia kwenye tamasha langu lililokuwa linaitwa
Wakilisha. Nilimlipa dola 3,000, baada ya kupokea fedha, hakuonekana
tena na hata simu yangu akawa hapokei.
No comments:
Post a Comment