Wafupishwa kwa muda ili kukabiliana na tishio la usafiri na mvua.
Mashindano ya Olimpiki ya 2012 jan usiki yalizinduliwa rasmi jana huku Tanzania ikiwakilishwa na wanamichezo sita.Sherehe hizo zilizoghrimu paundi milioni 27 zilifupishwa kwa muda wa dakika 30 kuhofia watu kukosa usafiri kutokana na hofu ya kunyesha mvua lakini kulikuwa na manyunyu tu.Mashindano hayo yaliyoshirikisha mataifa 250 kutoka ulimwenguni kote yameweka rekodi kwa kila taifa linaloshiriki kuwa na washiriki wa kike. Macho na masikio ya watu wengi yapo katika mchezo ya mbio fupi ambapo taifa la Jamaika litakuwa katika vita kali kati ya Usain Bolt na Yohane Blake...... na pia katika soka ambapo michezo hiyo ilianza tangu jumatano ambapo taifa la brazili linaonekana kutaka kufanya vizuri .Katika mashindano hayo tani saba za dhahabu,shaba na fedha zilizochimbwa Mongolia na Utah zitatumika kuwatunza washindi huku zikiwa chini ya ulinzi mkali chini ya jumba la malikia.
Angalia video ya ufunguzi wa Olimpiki ya London 2012
No comments:
Post a Comment