Hii ni picha na maneno ya kuomba radhi yanayodaiwa kutolewa na Eric
Shigongo ambayo yamewekwa kwenye mtandao wa Uganda, ikiwa ni propaganda
za kitoto za Chameleone za kujaribu kujikosha kwa mashabiki zake. Awali,
picha na maneno haya yaliandikwa kwa Kiswahili kibovu na kuwekwa kwenye
Fan Page ya Chameleone kwenye facebook, alipoona watu wameshitukia
Kiswahili kibovu kilichotumika ambacho hakiwezi kuwa cha Shigongo,
wakaamua kuondoa pamoja na taarifa zingine za kipuuzi alizokwisha weka.
Hivi sasa picha hii imebadilishwa na kuandikwa kwa Kiingereza cha
Kiganda na kisha kuwekwa kwenye mtandao wa Uganda, mtaona ni kiasi gani
zinafanyika kampeni za kutaka kumsafisha Chameleone ambaye alishachafuka
siku nyingi! Shigongo HAS NEVER, AND HE NEVER APOLOGISE TO 'Dr. Jose
Chameleone'!
No comments:
Post a Comment