MAHAKAMA YA MAPENZI
Wednesday, August 15, 2012
MADAKTARI WAMSTAAFISHA MUAMBA
Fabrice Muamba ameambiwa na madaktari kuwa anastahili kustaafu soka na Bolton wanatarajia kutangaza rasmi taarifa hizo.Muamba aliyesafiri kwenda Ubelgiji kwaajili ya upasuaji mdogo wa moyo ameshauriwa kuchukua uamuzi kutokana na hali yake kuonekana haijatengemaa....Muamba aliyeanza maisha yake ya soka katika timu ya Arsenal kisha Birmigham Kabla ya kwenda Bolton kwa Paund milioni 5 alianguka uwanjani katika uwanja wa White Hert Line tarehe 17 march huku moyo wake ukisimama kwa dakika 78....
Fabrice Muamba alikimbilia Uingereza pamoja na baba yake akiwa na umri wa miaka 11 kuikimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa ikiendelea nchini humo...Hata na hivyo kiungo huyo hakuwahi kuchezea timu ya Congo ila ameshachezea timu ya vijana ya Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment