Professor Jay(The Heavy Weight MC) ameamua kuingiza
mtaani(kupitia kila aina ya media inayoweza kuwafikia wananchi na
mashabiki wa muziki) single inayokwenda kwa jina Hellow. Hii inakuwa single ya tatu kutoka katika album ya JaySco Dagamaambayo
ingawa bado hajaamua kuitoa rasmi,ni wazi kabisa kwamba pengine itakuwa
album bora kabisa kuwahi kutolewa nchini Tanzania na msanii kutoka
kizazi kinachoitwa “Kizazi Kipya” au New Generation.
Hellow unatoka katika kipindi muafaka.Kama unafuatilia sindimba za
starehe nchini Tanzania,kilichopo kwenye kona ni msimu mnene wa Fiesta.Hellow,bila shaka,inalenga katika kuhakikisha kwamba,mtaani kila mtu anamwambia mwenzake Hellow.
Hii ni production kutoka kwa Dully Sykes ambaye bila shaka
utakubaliana nami kwamba ameitendea haki vilivyo chorus ya wimbo
huu.Usikilize Hellow;Cheki juu kudownload....
No comments:
Post a Comment