Search This Blog

Nyumbani-Kigoma All stars

MAHAKAMA YA MAPENZI

Wednesday, June 27, 2012

DOKTA ULIMBOKA ATEKWA APIGWA YUPO ICU

 Hii picha ikimuonesha Dr Ulimboka baada ya kuokotwa....
Dr Ulimboka akiwa katiak moja kati ya mikutano ya madaktari
Kiongozi wa madaktari Dr Steven Ulimboka  ameokotwa leo asubuhi eneo la msitu wa Mwabe pande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam  huku akiwa ameumia vibaya sana.Mpaka tunarusha taarifa hii inasemekana Dr Ulimboka yupo icu katika hospitali ya taifa Muhimbili huku akiwa hapumui vizuri...Dr ulimboka anayejulikana kwa misimamo yake na kupigania haki za madaktari alitekwa majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo na inasemekana amevunjika pia mkono,taya na kuumia vibaya sehemu nyingine za mwili wake...Wakati haya yakijiri serikali kesho itatoa msimamo juu ya mgomo wa madaktari unaoendelea kwa baadhi ya hospitali....Get well soon mpambanaji  Ulimboka

Wednesday, June 20, 2012

P-Square ft Rick Ross-Beautyfull Onyinye

Peter na Paul Okoye mapacha wa kinigeria wameendelea kuudhirishia uma wa mashabiki wa muziki duniani kuwa ni moto wa kuotea mbali mara baada ya video yao mpya ya Beautifull  Onyinye  waliomshirikisha bosi wa lebo ya Maybach Rick Ross kuwa hewani na kufanya vizuri ajabu......P square ambao wamekuwa na mlolongo wa mafanikio ikiwamo kusaini mkataba wa kuwa chini ya lebo ya Convict iliyochini ya msenegali anayetesa kimataifa  Akon,kusaini  mkataba na kampuni ya kusambaza kazi za mziki ya Sony kwa kusambaziwa kazi zao ulimwengu mzima pamoja na kununua ndege mpya ya kisasa kwa ajili ya kazi zao...Ngom hiyo yenye mahadhi kama yale ya no one like you inaanza kwa mtu mzima ross kuitambulisha lebo ya convict na baadae ni Maybach...Pia Rick ross ameonesha uwezo mkubwa sana katika kuchana ndani ya beat hiyo iliyokaa kiafrika zaidi.Big up P-Square.

Monday, June 18, 2012

AY NA FA WAFANYA MAKAMUZI BBA

Wanamuziki wa kitanzania wameendelelea kuonyesha kuwa ni lulu nje ya mipaka ya Tanzania baaada ya jana   AY na FA  kufanya show ya nguvu ndani ya mjengo wa BBA....Hili limekuja siku chache baada ya mtumbuizaji bora wa tuzo za KTM Diamond naye kukamua vibaya sana ndani ya Jumba la kaka mkubwa aka BIG BROTHER....
AY  na  mwenzake FA ambao majuzi walitangaza kujitoa  katika lebo ya B hitzz chini y produza Hermmy B walisahau migogoro yao na mabosi wao wa zamani na kuwapagawisha vilivyo watu watu walihudhuria show hiyo bondeni kwa mzee Madhiba.
Kwa mtazamo wetu sisi wanacommunity tunaamini mziki wetu umekuwa na ndio maana mialiko hiyo inazidi kuwa mingi hivyo tunawataka wakaze buti na wasibweteke kwa mafanikio hayo waliyoyapata.

HATMA YA DOGO JANJA

Msanii wa bongo flava aliyekuwa kwenye utata na mabosi wake wa Tip top Connection Dogo janja ambaye alhamis alitua rasmi jijini Arusha na kutema cheche juu ya kile alichofanyiwa na kiongozi wa wa kambi ya Tip top iliyo na maskani yake  Manzese jijini Dar-es-salaam.
Siku ya ijumaa Dogo Janjaro akiwa ndani ya studio za radio 5 katika kipindi cha funiko base   kinachoendeshwa na Mc Julias Kamafa na kwanza alimtaka presenter huyo kumpigia simu mama yake mzazi ambaye alielezea vitu alivyokuwa akifanyiwa na  Ma dee ikiwemo kupigwa na kudhalilishwa.....
Kwa muujibu wa dogo janja mwenyewe siku moja kabla ya tukio alipigiwa simu na madee na kuombwa kwenda kwenye show kibaha kwa mshkaji wa madee kwa malipo ya shilingi laki moja  na aliporudi alfajiri alitakiwa kwenda shule kuchukua namba ya mtihani ila