Ngassa alikuwa mmoja wa wachezaji wa Simba waliokuwa mazoezini kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Mashabiki kibao walijitokeza kumshuhudia kiungo huyo ambaye amejiunga Simba kwa kulipwa dau la Sh milioni 30 pamoja na gari aina ya Toyota Verossa lenye thamani ya Sh milioni 18.
Baadhi ya mashabiki waliokuja eneo la tukio ni vijana waliokuwa katika mlolongo wa kuwania kushinda shindano la muziki la BSS zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo.
Ngassa alionekana kuwa mwenyeji tu na alifanya mazoezi vizuri kwa ushirikiano na wenzake. Mazoezi hayo yalikuwa chini ya Kocha Msaidizi, Richaed Amatre raia wa Uganda.
Simba imeilipa Azam kitita cha Sh milioni 25 ili kumchukua Ngassa ambaye amekuwa akidai hana raha .
Cheki page ya sports kwa picha zaidi
No comments:
Post a Comment